Diaspora - Roma, LADY JAYDEE

Diaspora - Roma, LADY JAYDEE

Год
2020
Язык
`Svahili`
Длительность
206260

Şarkının sözleri aşağıdadır Diaspora , sanatçı - Roma, LADY JAYDEE çeviriyle birlikte

" Diaspora " şarkısının sözleri

Çevirili orijinal metin

Diaspora

Roma, LADY JAYDEE

Ooii Yooh

Tongwe Records Beiby

(Bin Laden)

Umwambie sikupenda, kuikimbia nchi yangu

Kabla kalenda nimeondoka kabla ya mwanangu

Na sijui ninapokwenda simjui na mrithi wangu

Usije ukambemenda mwanangu oii

Kitovu chake ukizike nilipopitisha unyayo

Akiwa wa kike ndo furaha niitakayo

Ukinizalia dume Inshallah ni hayo

Nitampa jina la mtume na nitamuita Matayo

Akikuwa mwambie babake alikuwa mwanaharakati

Na ukamwonyesha ununio ndio kumbukumbu iliyobaki

Awaheshimu nduguze ambao walimwachia ziwa

Wamthamini wamtunze abadani asijione mkiwa

Na asinichukie mimi maana sikumchukia babu yake

Akikuwa atajua kwanini na ataheshimu maamuzi yake

Auchunge ulimi aishike dini yamkini ana jini mkongwe

Na umsikizishe yangu mapini (Ili mjini asikae kinyonge)

Na ukipata usimsahau mama, mkumbuke na bibi

Niombee nitusue mnyama, nabeba kago msumbiji

Sijui nitapona nitakufa sijui nitarudi

Akikuwa mwambie Roma ndo baba we ndo shahidi

Uvumilie, utuli, umlilie

Haya maisha ni safari

Usilie, uvumilie, utuli na umlilie

Haya maisha ni safari

Nafahamu utazaa kwa uchungu

Leba utalia na mengi akidondoka chini ya uvungu

Watambeba malaika wengi

Mimba huja na kisirani, na kuna unavyotamani

Huku nilivokuta sivo nilivodhani ila siwezi rudia njiani

Na unafahamu hunnie ile nyumba ya urithi haina vigae

So unaweza pima mzani ni rudi ama nikomae

Bora nikomae tu tujichange tumjengee mama kibanda

Inshallah mpaka uzae nitakuwa nimeshajipanga

Na nimetuma picha yangu waonyeshe wanangu wasinisahau

Waambie baba atarudi uwape moyo angalau

Kuna muda nina hamu ya ngono ila sina hisia ya mapenzi

So please ongeza visomo kwa yule Ustadh wa Mbezi

Najua unanimiss ila jitunze nami nitakutunzia fimbo

Walinde wanangu wao ndo warithi na ndizo za Roma simbo

Wananiambia mashabiki Roma rudi uchukue jimbo

Huku ukizingua polisi tu unaekewa goti la shingo

Basi ni hayo tu maisha ni mapambano ila sio sinza

Na usisahau kuwapa tano Dajide, Mada na Siza

Na uwaambie huku watu hawachagui kazi

Ila majungu na umbea yaani vitu ni vingi mzazi

Uvumilie, utulie, umlilie

Haya maisha ni safari

Usilie, uvumilie, utulie na umlilie

Haya maisha ni safari

Uvumilie, utulie, umlilie

Haya maisha ni safari

Tongwe Records Beiby

(Bin Laden)

2 milyondan fazla şarkı sözü

Farklı dillerde şarkılar

Çeviriler

Tüm dillere yüksek kaliteli çeviriler

Hızlı arama

İhtiyacınız olan metinleri saniyeler içinde bulun